Mtihani wa Taifa wa kuhitimu kidato cha nne na wa maarifa maarufu kama QT, unaanza kesho kote nchini, katika shule za sekondari 4,873 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 1,072.

Katika sehemu ya taarifa kwa umma iliyotolewa na baraza la Taifa la mitihani (NECTA), kupitia kwa Katibu mtendaji wake Daktari CHARLES MSONDE, katika mtihani huo watahiniwa wa kujitegemea wenye mahitaji maalum wako 384 ambapo wenye uoni hafifu ni 368 na wasioona ni 16.

Mtihani wa Kumaliza elimu ya msingi mwaka 2017/18 uligubikwa na vitendo vya udanganyifu wa mitihani ulioshirikisha mtandao wa watumishi wasio waamifu wa umma, wamiliki wa shule na walimu husika na katika taarifa yake, Dokta Msonde, ametoa angalizo juu athari za vitendo hivyo kujirudia katika mtihani huu wa kidato cha nne.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo limewaomba wananchi kutoa taarifa kwake na mamlaka nyingine ikiwemo za usalama, pale watakapobaini harufu yoyote ya hujuma dhidi ya mtihani huo utakaofanyika mpaka tarehe 25 mwezi huu.

Tazama Video Hapa Chini;

Comments

comments