Chama cha msalaba mwekundu Tanzania (TRC) leo kimezindua kampeni ya elimu kuhusu matumizi sahihi ya nembo za chama hicho baada ya kuwepo hujuma za ukiukwaji wa matumizi ya nembo hizo

Chama cha msalaba mwekundu Tanzania (TRC) leo kimezindua kampeni ya elimu kuhusu matumizi sahihi ya nembo za chama hicho baada ya kuwepo hujuma za ukiukwaji wa matumizi ya nembo hizo sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi.

Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Julius Kejo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo jijini DSM, amesema endapo wananchi watapata elimu sahihi kuhusu huduma za chama hicho cha msalaba mwekundu itasaidia kuongeza thamani ya alama hizo na huduma zinazotolewa na wanachama wake wakati wa majanga mbalimbali ya dharura.

Katika uzinduzi huo uliohudhuriwa na Mwenyekiti wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu Bi. Andrea Health, Bw. Kejo ametaja baadhi ya ukiukwaji unaofanywa kuwa ni pamoja na wenye hospitali na maduka binafsi ambao kubandika nembo hiyo na wahalifu wa kivita hutumia nembo hiyo kwenye magari yao kupitisha silaha.

Chama cha msalaba mwekundu Tanzania ‘TRC’ ambacho kilijiunga na shirikisho la vyama vya msalaba nwekundu duniani ‘IFRC’ mwaka 1963, kinatumia alama za msalaba mwekundu, hilali nyekundu na fuwele nyekundu, zikiwa ni alama za kuleta matumaini kwa watu waliokumbwa na majanga mbalimbali yakiwemo ya asili, migogoro kibinadamu na ya kivita, katika kuashiria kwamba msaada upo karibu.

Comments

comments