NAIBU WAZIRI ATAKA WALIOPEWA ARDHI KIHALALI WASISUMBULIWE

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula ameviagiza vyombo vya dola kuwachukulia hatua za kisheria watu wanaowabugudhi wananchi waliopewa maeneo kihalali kwani wanapaswa kufuata sheria endapo wanaona hawakutendewa haki na si kuchukua sheria mkononi.

Naibu waziri Angelina Mabula ametoa kauli hiyo akiwa katika ziara yake kikazi mkoani Tabora baada ya kutembelea eneo la mpera kata ya uledi mjini Tabora, eneo ambalo limekuwa na mgogoro wa muda mrefu

Anasema pamoja na serikali kusimamia utatuzi wa mgogoro huo na baadhi ya wananchi kupewa maeneo kihalali bado wapo ambao hawajakubaliana na maamuzi hayo, na kutaka kujipatia maeneo kinyume cha utaratibu

Awali naibu waziri alielezwa kuwa katika eneo hili kulikuwa na makubaliano kati ya wananchi na kampuni iliyokuwa ikifanya urasimishaji wa ardhi, kuwa baada ya urasimishaji asilimia sitini ya kila eneo litabaki kuwa mali ya mwananchi huku asilimia arobaini ikiwa mali ya kampuni pamoja na halmashauri kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo jambo ambalo baadhi yao hawakukubaliana nalo na hivyo kuibua mgogoro.

Katika hatua nyingine naibu waziri amekagua ofisi ya Ardhi wmanispaa ya Tabora na kubaini ucheleweshaji Katika utoaji hati na hivyo kuagiza Afisa Ardhi mteule wa manispaa Daud Msinge kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Comments

comments