Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Bw. Mussa Sima amesema ameridhishwa na utunzwaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji vinavyoelekea katika Bonde la Mto Rufiji na kuagiza mamlaka husika kuendelea kuvilinda kwa gharama zote.

Akizungumza katika eneo utakapojengwa mradi wa umeme wa ‘Stigler’s Gorge’ akiambatana na wajumbe Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) iliyokwenda kujionea namna mradi huo utakavyotekelezwa pasipo kuleta athari zozote za kimazingira, Waziri Sima amesema ziara yake ya kukagua na kuangalia vyanzo vya maji maeneo mbalimbali hapa nchini imekuwa ya mafanikio makubwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya NEMC, Profesa Esnati Chaggu amesema ziara waliyofanya imewajengea uwezo mkubwa kwani wameona na kujifunza vitu vingi katika maeneo waliyopita na kuwa kwenye nafasi nzuri ya kuisimamia menejimenti.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt.Samuel Gwamaka amesema ziara ya Bodi kutembelea Bonde la Mto Rufiji ina maana kubwa kwa wamepata nafasi ya kujionea jinsi hatua mbalimbali za kimazingira zilivyowezakuchukuliwa sambamba na utunzaji wa mazingira.

Naibu Waziri Sima katika ziara yake imemfikisha katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya na Morogoro na kuhitimishwa katika katika Bonde la mto Rufiji eneo litakapojengwa bwawa la kuzalisha umeme wa maji kiasi cha Megawati 2,100.

Comments

comments