NEMC KUFUATILIA UZALISHAJI WA VIFUNGASHIO

Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC limepanga kuvifuatilia viwanda vyote vinavyozalisha vifungashio ili kujiridhisha iwapo vinafuata taratibu na sheria ya matumizi ya vifungashio hivyo, ambavyo katika baadhi ya maeneo, watu wamegeuza matumishi yake na kuwa vibebeo vya bidhaa mbalimbali.

Akizungumza na Channel Ten katika mahojiano maalum jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja wa Baraza hilo Kanda ya Mashariki Mhandisi Benjamin Mchwampaka amesema tayari zoezi la kutoa elimu kwa wadau ikiwa ni pamoja na kwenye masoko yote limefanyika na hivi sasa wamejipanga kufanya ufuatiliaji kwa wazalishaji ambao baadhi yao wamekuwa wakiwapotosha wananchi kuhusu matumizi ya mifuko hiyo.

NEMC inachukua hatua hiyo ikiwa ni zaidi ya miezi miwili tangu serikali ilipopiga matumizi ya mifuko ya plastiki, agizo ambalo lilipokelewa vizuri na wananchi ingawa kwa sasa kumeibuka kuzagaa kwa mifuko myeupe katika mitaa na maeneo mbalimbali.

Comments

comments