Polisi nchini Kenya wamesema kundi la watu wasiojulikana waliojihami wamemteka mwanamke mfanyakazi wa shirika la misaada, raia wa Italia kutoka kusini mashariki mwa Kenya.

Watu hao wanaoarifiwa kujihami kwa bunduki, “wamefyetua risasi kiholela” kabla ya kumteka msaidizi huyo mwenye umri wa miaka 23 nje ya mji wa pwani Malindi.

Watu watano pia wanaarifiwa kujeruhiwa na wamepelekwa hospitalini, mmoja kati yao akiwa yuko katika hali mahututi.

Hata hivyo polisi wamesema haijajulikana wazi sababu za kutekeleza shambulio na bado uchunguzi unaendelea kufanya na jeshi la polisi.

Comments

comments