Kazi ya Ujenzi wa Majengo ya Rada inaendelea katika vituo mbalimbali, ambapo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam ujenzi umekamilika na tayari mtamnbo wa rada wa kituo hicho umeshaingia nchini na unatarajiwa kufungwa wakati wowote.

Hayo yamebainishwa kwenye semina ya waandishi wa habari na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA Bw Mbottolwe Kabeta, wakati alipokuwa akizungumzia mradi mkubwa wa kufunga rada mpya za kisasa katiak viwannja vya ndege vinne hapa nchini.

Amesema mradi huo utapokamilika utachangia kuongeza mapato yanatokanayo na tozo za kuongozea ndege,hatua itayochangia mapato ya serikali.

Mamlaka ya Usafiri wa anga Tanzania inafanya shughuli mbalimbali za kuelimisha umma kuhusu sekta ya usafiri wa anga, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Kimataifa ya usafiri wa anga.

Comments

comments