Rais Magufuli ahitimisha ziara ya siku 6 Arusha, Aahidi kuendelea kutatua kero za wananchi

IMGS2065

Rais John Pombe Magufuli leo amemaliza ziara yake ya siku 6 katika Mkoa wa Arusha.

Akiwa njiani kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) ,Rais Magufuli amesimamishwa na wananchi wa Sangsi , nje kidogo ya Jiji la Arusha na wananchi wa Pacha ya Kia Mkoani Kilimanjaro na kuwahakikishia kuwa Serikali itaendelea kutatua kero za wananchi na kuwahudumia bila kuwabagua kwa misingi ya itikadi za kisiasa, dini na ukabila.

Rais Magufuli amesema katika kutimiza azma hiyo , Serikali inatekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya Usa River ñ Arusha inayojengwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 139, mradi wa maji wa Arusha utakaogharimu Shilingi Bilioni 42, mradi wa kusambaza umeme katika vijiji zaidi ya 200 na mingine mingi inayotekelezwa katika maeneo hayo.

Aidha, Rais Magufuli amesikiliza kero mbalimbali za wananchi wakiwemo wafanyakazi ambao wamelalamikia kuhamishwa vituo vya kazi bila kulipwa stahiki zao na amerejea agizo lake la kupiga marufuku mfanyakazi yeyote kuhamishwa kituo cha kazi pasipo kulipwa stahiki zake.

Kuhusu kero za wananchi wa pacha ya Kia waliolalamikia tatizo la uhaba wa maji, kunyangíanywa maeneo ya biashara na waliokuwa walinzi wa uwanja wa ndege kudai haki zao , Rais Magufuli ameziagiza mamlaka husika kushughulikia matatizo hayo.

Comments

comments