Rais Dkt. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bw. Apson Mwangíonda, Ikulu Jijini Dar es salaam.

Baada ya mazungumzo hayo Bw. Apson Mwangíonda amemshukuru Rais Magufuli kwa kukubali ombi lake la kumuona na kuzungumza naye na amempongeza kwa uongozi mzuri unaochochea kasi ya maendeleo hususani katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo.

Bw. Apson Mwangíonda ameitaja baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo kuwa ni mradi wa uzalishaji wa umeme katika mto Rufiji (Stieglersí Gorge Power Project) na Ujenzi wa madaraja na barabara ambazo licha ya kurahisisha usafiri zitasaidia kuondoa msongamano wa magari katika Jiji la Dar es salaam.

Ametoa wito kwa wana nchi kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Awamu yaTano il iitekeleza mipango yake kwa ufanisi na kwa manufaa ya Taifa.

Comments

comments