Rais Magufuli, kesho anatarajiwa kukabidhi Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

Rais Dkt John Pombe Magufuli, kesho anatarajiwa kukabidhi Mfumo wa Usimamizi wa Mawasiliano ya Simu (TTMS) kwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA mfumo ambao utawezesha mambo mbalimbali ikiwemo Upatikanaji wa takwimu za mawasiliano ya Simu yanayofanyika ndani na nje ya nchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA Mhandisi James Kilaba amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa Mfumo ambao ulianza kufanya kazi rasmi Octoba Mosi mwaka 2013 mbali ya kuweza kusimamia shughuli nyingi zaidi kutokana na mazingira na mabadiliko ya teknolojia mpya zinapojitokeza pia utajikita katika mambo mbalimbali ikiwemo kugundua mawasiliano ya simu za ulaghai, kutambua mapato na takwimu za miamala ya fedha mitandaoni pamoja taarifa za laini ya simu na namba tambulishi za kifaa cha mawasiliano ikiwemo kusimamia kwa ufanisi ubora wa huduma za mawasiliano ili kuboresha viwango vya huduma hizo.

Viongozi na wananchi mbalimbali ambao ni wadau wa sekta ya mawasiliano wapatao 1500 wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo ya makabidhiano ya mfumo huo wa Mawasiliano, itakayofanyika Makao Makuu ya Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano jijini Dar es Salaam.

Comments

comments