Rais Dkt.John Pombe Magufuli, leo ameshuhudia makabidhiano ya mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu kutoka kwa makandarasi waliotengeneza mfumo huo ambao umekabidhiwa kwa Mamlala ya Mawasiliano Tanzania TCRA.

Rais Dkt.John Pombe Magufuli, leo ameshuhudia makabidhiano ya mfumo wa usimamizi wa mawasiliano ya simu kutoka kwa makandarasi waliotengeneza mfumo huo ambao umekabidhiwa kwa Mamlala ya Mawasiliano Tanzania TCRA wenye lengo la kudhibiti huduma za mawasiliano na kukabiliana na changamoto zinajitokeza kutokana na mabadiliko ya teknolojia.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kutiliana saini mkataba wa makabidhiano Rais Magufuli amesema mchahakato wa utengenezwaji wa mfumo huo ulighubikwa na changamoto nyingi ikiwemo baadhi ya watu kutoutaka na hivyo kukwamisha kwa makusudi juhudi hizo wakishirikiana na baadhi ya watendaji wa umma hatua ambayo ilimlazimu kuwaondoa baadhi ya watendaji wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA.

Rais Magufuli amesema sekta ya mawasiliano ni nyeti ambayo inagusa moja kwa moja ukuaji wa uchumi wa nchi hivyo ameitaka TCRA kuhakikisha inasimamia na kuutunza mfumo ili uweze kuleta tija.

Katika hatua nyingine Rais Magufuli amemuagiza waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mhandisi Issack Kamwelwe kuhakikisha taasisi zote za serikali ambazo hazijaingia kwenye mfumo wa serikali wa malipo wa kielektroniki – GePG zinajiunga ambapo amesema ni taasisi 339 kati 667 ndizo zilizojiunga na mfumo huo.

Akizungumzia faida za uwepo wa mfumo huo Mkurugenzi Mkuu TCRA Mhandisi James Kilaba amesema utasaidia upatikanaji wa takwimu za mawasiliano ya simu ndani na nje ya nchi,kubaini mawasiliano ya simu ya ulaghai, kutambua mapato na takwimu za miamala ya fedha mtandaoni ambapo tangu kuanza kutumika mapato yamepanda kutoka shilingi trilioni 8.5 hadi trilioni shilingi 11.6 kwa mwezi na kutaja mfumo huo kuwa chanzo kingine cha mapato.

Comments

comments