Secretarieti ya SADC yazindua machapisho matano.

Secretarieti ya Jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC leo imezindua machapisho matano yaliyobeba maudhui mbalimbali kuhusiana na sera, mipango na mikakati ya jumuiya hiyo.

Machapisho hayo ni pamoja na Mkakati wa kanda ya SADC kuhusu wanawake, amani na ulinzi (2018), Ufuatiliaji wa SADC katika masuala ya maendeleo ya jinsia (2018), Mkakati wa kanda ya SADC wa kuangalia ukatili wa kijinsia, Ufuatiliaji wa SADC katika masuala ya nishati na Tathimini ya mpango mfupi wa uendelezaji miundombinu kikanda 2019.

Akizungumza katika uzinduzi wa machapicho hayo, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, amezungumzia pamoja na mambo mengine namna ambavyo Tanzania imejikita katika kuhakikisha inafikia usawa wa asilimia 50/50 wanawake na wanaume katika ngazi za maamuzi ambapo mpaka sasa imefikia asilimia 37.

Naye Katibu Mtendaji wa SADC, Stergomena Tax, amesema mpaka sasa ni nchi mbili tu za SADC ambazo zimefikia asilimia 50/50 kati ya wanawake na wanaume katika ngazi ya maamuzi ambazo ni Afrika Kusini na Sychelles.

Nae Waziri wa Nishati Medard Kalemani aliyehudhuria uzinduzi huo uliokuwa na chapisho la Ufuatiliaji wa SADC katika Nishati 2018, ambayo inaonyesha kuwepo kwa uhaba wa mafuta, gesi na nishati ya umeme katika ukanda huo, ambaye amejinadi namna ambavyo Tanzania imejaaliwa katika sekta ya nishati na inajizatiti katika uzalishaji wa umeme ukiwemo wa gesi asilia na mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere katika bonde la mto rufiji.

Awali wakizungumzia umuhimu wa kuanzishwa kwa machapisho hayo wadau kutoka Kituo cha utafiti cha kusini mwa Afrika wameainisha pia changamoto zilizopo katika ukanda huo, ikiwemo ya mipango ya kikanda na kitaifa kutohuishwa pamoja na ushirikishwaji mdogo wa sekta binafsi.

Comments

comments