Serikali ya Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba imewatoa hofu wananchi kwamba dawa za malaria zinazopigwa majumbani mwao hazina madhara kwao, bali zimelenga kuangamiza mbu wanaoeneza malaria.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Bi Salama Mbarouk Khatib wakati akizungumza na wananchi wa shehia ya Tumbe ambao wamegoma kupigiwa dawa majumbani mwao.

Amesema lengo la serikali ni kutokomeza ugonjwa wa malaria ambapo ameahidi kusimamia zoezi hilo ili kuhakikisha linafanikiwa na nyumba zote zinapigwa dawa.

Afisa kutoka kitengo cha Malaria wizara ya afya Pemba Bakar Omar Khatib amesema wanachokifanya wanapofika kwenye nyumba ni kuwataka wakaazi wake kukunja vitu ambavyo vinaweza kuharibika ama kuathiriwa na dawa hiyo, huku Mratibu wa Mradi wa upigaji dawa Faki Haji Faki akiwahamasisha wananchi kuukubali mradi huo.

Zoezi la upigaji wa dawa linafanyika katika shehia ambazo zimegunduliwa kuwa na kesi za watu kuwa na virusi vya ugonjwa wa malaria.

Comments

comments