Serikali imeruhusu wafanyabiashara wenye vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kuendelea kufanya hivyo siku chache tangu wizara ya kilimo kueleza nia yake ya kusitisha uagizaji wa sukari kutoka nje kwa wazalishaji wa ndani.

Serikali imeruhusu wafanyabiashara wenye vibali vya kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kuendelea kufanya hivyo siku chache tangu wizara ya kilimo kueleza nia yake ya kusitisha uagizaji wa sukari kutoka nje kwa wazalishaji wa ndani, baada ya majadiliano kati ya wazalishaji hao na wizara ya kilimo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam waziri wa kilimo Japhet Hasunga amesema katika majadiliano hayo wazalishaji wa ndani wameihakikishia serikali juu ya uwezo wao wa kuongeza uzalisha sukari kufikia tani laki 345 kwa mwaka kutoka laki 320 za awali huku upungufu ukiwa ni Tani elfu 30 kwa mwezi, hivyo serikali ikaona haina haja ya kuendelea na katazo hilo

Hata hivyo waziri Hasunga amesema mahitaji ya sukari kwa mwaka ni tani laki 670 hivyo upungufu huo utaendelea kuagizwa na wazalishaji kwavile hapa nchini ni viwanda vinne tu ndio vyenye uwezo wa kuzalisha tani laki 345 za sukari ya matumizi ya nyumbani pekee huku ya viwandani ikiwa bado ikiagizwa kutoka nje ya nchi kwa asilimia 100 kutokana na kutokuwepo na viwanda vya kuzalisha sukari hiyo.

Aidha amebainisha kuwa bodi ya sukari imefanya utafiti na kubaini kuwa zipo tani laki moja ishirini na tisa elfu za sukari ya ziada ambayo itapunguza upungufu uliyopo hususani katika kipindi ambacho waumini wa dini ya kiislamu wanaelekea kwenye mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Waziri Hasunga ameweka bayana mipango ya serikali ya namna ya kukabiliana na upungufu wa sukari na inaendelea kukaribisha wawekezaji katika mashamba makubwa ya miwa na kufungua viwanda vya kuzalisha bidhaa hiyo.


Comments

comments