Shirika kuu la utangazaji la China CMG lajitahidi kufanya uvumbuzi na kujijenga kuwa chombo kikubwa cha habari cha aina mpya.

Shirika kuu la utangazaji la China CMG linajitahidi kutumia teknolojia mpya na kufanya uvumbuzi wa kuunganisha mbinu za kisasa za utangazaji kupitia majukwaa mbalimbali, ili kutangaza kwa ufanisi maamuzi ya Chama na maoni ya wajumbe kwenye Mikutano miwili inayoendelea kufanyika hapa Beijing.

Wakati wa kuripoti Mikutano mwili ya mwaka huu, Shirika kuu la utangazaji la China limetumia kwa mara ya kwanza teknolojia ya 5G katika kutangaza moja kwa moja matukio ya mikutano hiyo kwa picha zenye ubora wa 4K. Ili kuwaonyesha wajumbe wa mikutano hiyo mabadiliko yanayotokana na teknolojia mpya, shirika hilo pia limetumia teknolojia mbalimbali za kisasa ikiwemo 5G, Big Data na akili bandia kutoa huduma za televisheni ya 4K kwenye jumba la mikutano, kituo cha habari na hoteli wanazokaa wajumbe hao.

Shirika hilo pia limetumia nguvu yake bora ya video na sauti na kuunganisha majukwaa mbalimbali, ikiwemo CCTV, CNR, CRI na tovuti, kwa ajili ya utangazaji wa Mikutano Miwili.

Comments

comments