Shirika la Reli Tanzania limesema kuwa milango bado ipo wazi kwa makundi mbalimbali kuutembelea mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya SGR inayojengwa kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kwa lengo la kujifunza kama walivyofanya wasanii mbalimbali nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TRC Masanja Kungu Kadogosa mara baada ya kupokea wasanii,wanamichezo na washereheshaji zaidi ya 300 waliotembela mradi wam Ujenzi wa Reli hiyo ya kisasa.

Wasanii hao walitumia usafiri wa treni ya delux na kushuhudia ujenzi wa Reli hiyo wakiwa ndani ya treni hiyo ambapo pia walikuwa wakishuka na kujionea hali ya ujenzi huo.

Katika hatua nyingine Mkuu WA Mkoa WA Dar as salaam Paul Makonda ametoa rai kwa wananchi waendelee kutembelea miradi ambayo inatekelezwa na Serikali ya awamu ya tano ya Dokta John Pombe Magufuli.

Mmoja wa wasanii aliyejumuika katika safari hiyo Shafii omary akatoa neno baada ya kujionea ujenzi huo na kufuria safari hiyo.

Comments

comments