Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL limepewa siku 30 kuhakikisha maeneo yote ambayo hayana kadi za simu na vocha za simu za mtandao huo zinawafikia.

Akizungumza alipotembelea makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye amesema haifai kuona maeneo ya vijijini bado hayapati huduma za mawasiliano kwa ufanisi.

Naibu Waziri Nditiye ametoa mwezi moja kwa shirika hilo kutatua changamoto ya upatikanaji wa kadi za simu pamoja na vocha za simu katika maeneo ya vijijini.

Comments

comments