Shirika la viwango Tanzania TBS limeteketeza tani 4.5 za bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Milioni 67, baada ya kubainika kuwa na viwango hafifu vya ubora.

Bidhaa zilizotekezwa ni pamoja vifaa vya kuzuia majanga ya hitilafu za umeme na radi majumbani (earth copper), vijiko vinavyotumika kwa matumizi ya nyumbani kama vile kulia chakula, pamoja na makufuli ambavyo vilikamatwa February 2 mwaka huu katika bandari ya Dar es salaa vikiingizwa nchini kutokea China.

Afisa Ubora wa Viwango wa TBS Grangay Masala aliyesimamia zoezi hilo la kuteketeza akizungumza na waandishi wa habari walioshuhudia zoezi hilo anafafanua kuhusu uteketezaji huo.

Bw. Masala pia ameeleza kuwa ili kukabiliana na changamoto kutoka kwa wafanyabiashara wanaoingiza bidhaa zisizo na ubora kwenye soko la Tanzania, Shirika limeamua kubuni hatua mbalimbali za kudhibiti hali hiyo.

Mbali na hatua hizo za kukamata na kuteketeza bidhaa zisizo na ubora, TBS imekuwa katika mkakati wa kutoa elimu kwa wafanyabiashara na wazalishaji kuingiza ama kuzalisha bidhaa zinazokidhi matakwa ya bora ili kuepuka madhara na hasara, lakni pia kulinda ubora wa soko la Tanzania.

Comments

comments