Klabu ya Soka ya Simba imepata viongozi wake wapya baada ya kufanya uchaguzi wao leo viongozi ambao wataongoza kwa miaka minne huku ambapo Simba ikifanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza ikiwa katika hatua za mwisho kuelekea kukamilisha mchakato wa mabadiliko

Klabu ya Soka ya Simba imepata viongozi wake wapya baada ya kufanya uchaguzi wao leo viongozi ambao wataongoza kwa miaka minne huku ambapo Simba ikifanya uchaguzi huo kwa mara ya kwanza ikiwa katika hatua za mwisho kuelekea kukamilisha mchakato wa mabadiliko kutoka mfumo wa zamani wa wanachama kwenda kiuwekezaji.

Akizungumza awali kabla ya kufanyika uchagzui huo Kaimu wa Rais wa Simba ambaye amemaliza muda wake Salim Abdallah aliwaomba wanachama kuchagua viongozi walio bora na wenye maaadili sambamba na kuwakumbusha viongozi ambao wamepata nafasi za kuongoza klabu hiyo kibwa barani afrika.

Amewaasa viongozi hao wa ngazi mbalimbali ndani ya Klabu hiyo kuwatumikia wanachama wa Simba kwa kuwapa raha michezoni ikiwepo simba kutwa mataji mengi pamoja na kujiendesha bila hasara.

Swedy Mkwabi ambaye amepata ridhaa ya kuingoza Simba kwa kuchaguliwa na wanachama amesema kuwa nia yake ni kusaidia maendeleo ya Simba na kuwapa wanachama haki zao za msingi ikiwepo kuwafikia kwa wakati na kuwapa kadi ambazo zitakuwa zikiwasaidia kuwatambulisha ndani ya klabu hiyo kongwe.

Katika hatua nyingine Salim akatoa neno kwa viongozi hao kwa kuwaeleza kuwa dhamana waliopewa ni kubwa na wanapaswa kuitendea haki Simba na wanachama wenyewe ikiwepo kujiepusha na mambo ambayo yataashiria migogoro ndani ya klabu hiyo.

Uchaguzi huo alimanusura uingie dosari kufuatia malalamiko ya Mwanachama wa klabu hiyo Mwina Kaduguda ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya Ujumbe Klabu ya Simba kutolewa nje ya ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu JK Nyerere kufuatia kupinga kuongezeka kwa idadi ya wapiga kura zaidi ya 300 iliyotangazwa na Mwenyekiti wa Uchaguzi Boniface Lihamwike.

Kufuatia mtafaruku huo uliopelekea Kaduguda kutolewa nje wagombea wengine nao walitoka nje, wakiongozwa na Swedy Mkwabi wakitaka kuzungumza pembeni au nje ya ukumbi juu ya swala hilo la kutolewa kwa mwanachama huyo ambaye pia alikuwa mgombea.

Tazama Video hapa Chini;

Comments

comments