Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa -TAKUKURU imewaonya wananchi pamoja na watumishi wa Umma, na Serikali kujiepusha na Vitendo vya Rushwa, Utakatishaji fedha pamoja na Ufisadi kwani hivi sasa wana Mamlaka kamili ya Kutaifisha Mali za Watuhumiwa pindi Watakapothibitika wamejihusisha na Vitendo hivyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na TAKUKURU Kamishna wa Polisi Diwani Athumani amesema kutokana na sheria hiyo wananchi na watumishi wa Umma na serikali wanatakiwa kuchukua tahadhari. Kamishna Diwani amesema Takukuru kuanzia mwaka 2016-2019 imeingiza shilingi Billioni 14.9 kwa kutaifisha Mali za wala[…]