Tehama Shuleni, Halotel kuboresha Mradi wa Internet For School

HALOTEL

Kampuni ya simu za mkononi ya HALOTEL,imesema itaboresha zaidi progamu yake ya Halotel Internet For School, ambayo tayari imeshazifikia jumla ya shule 450 za sekondari nchini.

Meneja Mawasiliano wa HALOTEL, Hindu rashid amesema mradi huo ulioanza mwaka 2015, Halotel ilipoanza shughuli zake nchini,unalenga kuunga mkono jitihada za serikali za kuhakikisha Tehama inatumika kutoa elimu nchini ili kuziba pengo katika kufundisha na kujifunza.

Amesema,kampuni hiyo itazidi kuboresha hususani huduma ya Internet Fiber,inayotumika katika mradi huo kufuatia huduma hiyo kuleta matokeo chanya.

Afisa huyo,amesema,mradi huo licha ya kukumbwa na changamoto hususani katika baadhi ya maeneo,umekuwa na mafanikio hususan ya kuongeza viwango vya ufaulu katika shule ikiwamo shule ya Sekondari ya Lugoba,mkoani Pwani ambao kwa mujibu wa Hindu Rashid kabla ya kuanza kwake mwaka 2015,shule hiyo ilikuwa inashika nafasi ya 3,452 kitaifa lakini mwaka 2016,katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne imepanda kwa nafasi elfu moja na kushika nafasi ya 2,452.

Comments

comments