Teknolojia za kisasa kuleta mwelekeo mpya wa kuchanganywa kwa vyombo vya habari.

Vyombo vikuu vya habari vya China ikiwemo Shirika Kuu la Utangazaji la China vimetumia teknolojia ya kisasa katika kukusanya na kutangaza habari za mikutano ya Bunge la Umma na Baraza la Mashauriano ya kisiasa la China inayofanyika hapa Beijing.

Wajumbe wanaohudhuria mikutano hiyo wamesema, teknolojia hizo zitaleta mwekeleo mpya wa kuchanganywa na kuendelezwa kwa vyombo vya habari.

Mjumbe wa Bunge la Umma la China Bw. Lu Lin amesema, hivi sasa aina ya vyombo vya habari imeongezeka, na habari zinaweza kuwafikia wananchi kwa wakati zaidi. Mjumbe mwingine Bw. Wu Jian ambaye pia ni mkurugenzi wa maabara ya teknolojia muhimu za ulinzi wa taifa amesema, hii ni mara ya kwanza duniani kutangaza vipindi vya televisheni kwa njia ya 5G, ikimaanisha kuwa teknolojia ya 5G ya China imeanza kutumiwa kihalisi.

Mjumbe wa Baraza la Mashauriano ya Kisiasa la China Bi. Feng Lichao amesema, picha za televisheni ya teknolojia ya 5G zinaonekana vizuri zaidi, na teknolojia hiyo inapaswa kutumiwa zaidi haraka iwezekanavyo.

Comments

comments