Timu iliyoundwa kuchunguza chanzo cha ajali iliyotokea maeneo ya Senjele wilayani Mbozi mkoani Songwe na kusababisha vifo vya watu 19 February 21 mwaka huu imewasilisha ripoti yake ambayo imebaini kuwa chanzo kikubwa cha ajali hiyo ni ubovu wa lori ambalo lilikuwa likitokea nchini Zambia.

Ajali hiyo ilihusisha malori mawili na bus la abiria aina ya Coaster mali ya kampuni ya Komkya.

Akiwasilisha ripoti ya uchunguzi wa ajali hiyo iliyoundwa chini ya Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani nchini Fortunatus Musilimu, Katibu wa kamati hiyo KISBERT KAPONDO ametaja chanzo cha ajali hiyo ambayo iligharimu maisha ya watanzania 19.

Mkuu wa mkoa wa Songwe Brigedia Jeneral mstaafu NICODEMAS MWANGELA amepokea taarifa hiyo na kumtaka kamanda wa polisi mkoani humo, kuhakikisha wanafanya ukaguzi wa magari yote yanayosafiri masafa marefu na yanayotoka nje ya nchi ili kudhibiti magari mabovu kutembea barabarani kwani ajali nyingi zinasababishwa na ubovu na magari.

Channel Ten imetembelea kituo cha ukaguzi kwenye mizani ya Mpemba mjini Tunduma wilaya ya Momba, ambapo madereva waliokaguliwa wamesema wanaipongeza serikali kwa kuanza zoezi la ukaguzi wa magari yao hivyo wakaiomba serikali kufanya zoezi hilo liwe la kudumu ili kuzuia ajali zinazoweza kuzuilika.


(Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe GEORGE KYANDO amesema tayari askari wa kikosi cha usalama barabarani wameanza zoezi la ukaguzi wa magari yote na hivyo zoezi hilo ni endelevu na watafanya ukaguzi kwa masaa 24 kila siku)

ACP. GEORGE KYANDO -Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe

Comments

comments