Kuelekea uchaguzi mkuu DRC Congo,Kampeni zaanza rasmi leo.

Kampeni za uchaguzi mkuu Wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo zinaanza rasmi hii leo ikiwa ni hatua ya mwisho ya kuelekea uchaguzi huo uliopangwa kufanyika Desemba 23 mwaka huu.

Kampeni hizi zinaanza wakati wanasiasa wa nchi hiyo wanaoishi nje na walioruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huo wakiwa wameanza kurejea nyumbani kwa ajili ya kampeni za uchaguzi huo, miongoni mwao akiwemo Martin Fayulu Madidi ambaye aliteuliwa hivi karibuni na wapinzani katika mkutano wa Geneva, kupeperusha bendera ya Upinzani, ambapo wanasiasa wawili mashuhuri Felix Tshisekedi wa UDPS na Vital Kamerhe wa UNC waliondoa saini zao.

Kinyanganyiro kigumu kinachotarajiwa kushudiwa nchini humo ni kati ya Mgombea wa Upinzani Martin Fayulu na Mgombea mteule wa rais Joseph Kabila, ambaye anapeperusha bendera ya muungano wa vyama tawala FCC, Emmanuel Ramazani Shadary.

Wakati hayo yakijiri wanasiasa nchini DRC wanatofautiana kuhusu matumizi ya mashine za kupigia kura ambapo tume inayosimamia uchaguzi inakabiliwa na changamoto ya kuwahamasisha wananchi kuhusu uchaguzi kupitia mfumo wa elekroniki.

Comments

comments