Uingereza inaweza kupitisha uamuzi wa upande mmoja na kubatilisha mkataba wa kujitenga na Umoja wa Ulaya – Brexit.

Mwendesha mashitaka mkuu Manuel Campos Sanchez-Bordona amesema mbele ya Korti Kuu ya Umoja wa Ulaya mjini Luxembourg, kuwa masharti fulani yanairuhusu Uingereza kufanya hivyo.

Bunge la Uingereza limeanza majadiliano yatakayodumu siku tano kuhusu mustakbali wa mkataba wa Brexit.

Aidha wabunge wanatarajiwa kupiga kura Desemba 11 inayokuja kuamua kama waunge mkono au la mkataba huo wa Brexit.

Comments

comments