Ethiopia imesema imemkamata aliyekuwa Naibu Mkuu wa Idara ya Ujasusi nchini humo, baada ya Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuanzisha hatua kali wiki hii dhidi ya maafisa waandamizi wa usalama

Ethiopia imesema imemkamata aliyekuwa Naibu Mkuu wa Idara ya Ujasusi nchini humo, baada ya Serikali ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kuanzisha hatua kali wiki hii dhidi ya maafisa waandamizi wa usalama wanaotuhumiwa kwa ukiukaji wa haki za binaadamu na ufisadi.

Aidha shirika la habari la Fana la nchini humo hapo jana lilitangaza kukamatwa kwa mkuu wa kitengo cha usalama kwenye mtandao wa huduma za simu unalomilikiwa na serikali wa Ethio Telecom.

Zaidi ya maafisa 60 wamekamatwa tangu Jumatatu, miongoni mwao wakiwa ni wa idara ya ujasusi pamoja na baadhi ya watumishi wa kampuni kubwa ya kijeshi ya uhandisi na utengenezaji chuma METEC ambapo tayari baadhi yao wamefikishwa mahakamani.

Jaji anayesikiliza kesi zao, amekataa kuwapa dhamana na kuwapa polisi siku 14 za kufanya uchunguzi zaidi. Hakuna ambaye tayari amekwishafunguliwa mashitaka.

Comments

comments