Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Mazingira, Maelfu ya watu wafanya maandamano wakizitaka nchi za Ulaya kuweka hatua kali.


Wakati Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa mazingira COP 24, unaanza leo huko Katowice Poland, maelfu ya watu wameandamana mjini Brussels Ubelgiji wakitaka ulinzi zaidi wa mazingira.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari watu 65,000 wameandamana katika mji huo mkuu wa Ubelgiji ambapo waandamanaji hao wanataka serikali na nchi za Ulaya kuweka hatua kali za kulinda utoaji wa gesi chafu ya carbon.

Waandamanaji hao wanasema ni kwa njia hiyo tu ndiyo ulimwengu utaweza kupunguza kiwango cha joto duniani kwa sentigredi 1.5 na kuyafikia malenmgo ya mkataba wa mazingira wa Paris wa mwaka 2015.

Maandamano mengine pia yamefanyika katika miji mingine ya nchi za Ulaya kama vile Berlin na Cologne nchini Ujerumani.

Mkutano huo wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa unakuja katika wakati muhimu ambapo ongezeko la joto duniani linatishia kupotea kwa viumbe na uoto wa asili.

Tiyari Benki ya Dunia imeahidi kiasi cha Dola bilioni mia mbili kusaidia uwekezaji kwenye suala la mabadiliko ya hali ya hewa kwa mwaka 2021-25, na kuongeza kiasi hiki kwa mara mbili ya fedha zake za sasa za ufadhili wa miaka mitano.

Comments

comments