Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umesema hautamvumilia mtu au kikundi cha watu watakaotumia lugha ya matusi au udhalilishaji dhidi ya viongozi.

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa umesema hautamvumilia mtu au kikundi cha watu watakaotumia lugha ya matusi au udhalilishaji dhidi ya viongozi badala yake umetoa rai kwa wananchi kuunga mkono juhudi zinachukuliwa na serikali ya awamu ya 5 katika kuimarisha uchumi.

Akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya ujasiriamali kwa vijana mkoani Iringa yaliyofanyika katika Halmashauri ya wilaya ya Mufindi, M/Kiti wa UVCCM mkoa wa Iringa Kenan Kihongosi amesema katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na matumizi mabaya ya dhana nzima ya uhuru wa kujieleza hali ambayo imekuwa ikisababisha usumbufu ambao haupaswi kufumbiwa macho.

Kwa upande wake Mjumbe wa Halmashauri Kuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa kupitia Jumuiya ya Umoja wa Vijana, Mussa Mwakitinya amewataka wa Tanzania hususani vijana kuepuka kutumiwa katika mitaji ya kisiasa na baadhi ya wanasiasa wasio waadilifu kwani maendeleo ya kweli hayabagui mtu kwa misingi ya itikati za kisiasa.

Comments

comments