VIDEO : Zoezi la Kikaka lenye lengo la kujenga uwezo kwa askari na maafisa wa Kijeshi.

Zoezi la Kikaka lenye lengo la kujenga uwezo kwa askari na maafisa wa Kijeshi katika uwanja wa vita juu ya matumizi ya silaha na mbinu za kivita limekamilika ambapo Kikosi hicho cha 24kj Mkoani Kigoma kimetakiwa kuendelea kukagua na kutembelea maeneo yote ya mapori ambayo hutumiwa na baadhi ya watu kufanyia vitendo vya uhalifu na ujambazi wa kutumia silaha.

Akiahirisha zoezi KIKAKA kwa jeshi la wananchi Tanzania JWTZ mkuu wa Brigedi ya Magharabi 202kv Brigedia Jenerali Jacob Mkunda amesema ipo haja ya kuendelea kufanya zoezi hilo mara kwa mara ili kuhakikisha amani ya kutosha inakuwepo mkoa wa Kigoma na kuondokana na matukio ya mauaji yanayojitokeza kila kukicha jambo linalochangia vifo vya wananchi wasio na hatia.

Hali ya ujambazi imekuwa ikishamiri katika wilaya ya Kasulu Kibondo na Kakonko ambapo Mkuu wa wialya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala amesema ulizi dhabiti unaitajika katika wilaya hizo ambazo zipo maeneo ya mipakana huku Mkuu wa utendaji wa kivita kanda ya Magharibi Wilbold Ibuge akitoa pongezi kwa askari hao wa kikos cha 24kj.

Ukiachilia mbali ulinzi wa amani kwa wananchi lakini pia mkoa wa Kigoma Unavivutio ambavyo pia vinapaswa kulindwa pamoja na miundombinu mbalimbali ambapo aliyemwakilisha mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Kanali Saimon Anange ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kasulu anasema ulinzi dhabiti kwa ajili ya uendelevu wa ziwa Tanganyika unahitajika.

Tazama hapa Kwa Urefu zaidi;

Comments

comments