WAKENYA WAWAPA MBINU ZA KUPATA MASOKO YA PARACHICHI WAKULIMA NJOMBE

Wataalam wa masoko ya Maparachichi kutoka nchini Kenya wamewataka wakulima mkoani Njombe wanaojihusisha na kilimo hicho Nyanda za Juu Kusini kuunda vyama vikubwa ambavyo vitawawezesha kupata njia za kuuza mazao yao moja kwa moja katika masoko ya barani Ulaya tofauti na kutegemea nchi ya Kenya pekee ya kupata masoko ikiwemo kutumia mbinu za kugonga nembo ya utambulisho wa bidhaa kutoka Kenya…

Takribani wakulima 150 wa zao la matunda ya Parachichi kutoka mkoani Njombe wanaounda Kikundi cha Njombe Southern Highlands Association wamekutana na mtaalam kutoka nchini Kenya ambaye anajishughulisha na uandikaji wa maandiko ya kuomba ufadhili wa masoko ya Parachichi barani Ulaya na kubainisha changamoto zinazowafifisha kufikia lengo lao kwa sasa.

Ujio wa mtaalam kutoka nchini Kenya ambao umepokelewa kwa matumaini makubwa ya kubadilisha mbinu mpya za kupata masoko kama wakulima hao watazingatia ushauri waliopewa, mtaalam huyo anaelezea faida za kuwa na vikundi….

Mwenyekiti wa Kikundi cha Njombe Southern Highlands Association, Frank Msigwa anasema zaidi ya tani 3000 kwa mwaka wanekuwa wakizizalisha, lakini soko limekuwa ni kikwazo

Comments

comments