Wakati raia wa Nigeria wakisubiri kufanyika kwa uchaguzi mwishoni mwa wiki hii baada ya tarehe ya awali kuahirishwa, bado kumekuwa na kizungumkuti kufanyika kwa uchaguzi huo licha ya ya Tume ya Uchaguzi (INEC) kuwahakikishia kuwa Uchaguzi huo utafayika.

Wakati raia wa Nigeria wakisubiri kufanyika kwa uchaguzi mwishoni mwa wiki hii baada ya tarehe ya awali kuahirishwa, bado kumekuwa na kizungumkuti kufanyika kwa uchaguzi huo licha ya ya Tume ya Uchaguzi (INEC) kuwahakikishia kuwa Uchaguzi huo utafayika Jumamosi Februari 23, 2019.

Hata hivyo ikiwa zimesalia mbili kabla ya kufanyika uchaguzi huo, tume ya uchaguzi inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa baadhi ya kuongozi wa vyama wakitaka kujiuzulu kutokana na kutokuwa na imani na tume hiyo.

Baadhi ya viongozi wa vyama vinaishtumu Tume ya Uchaguzi (INEC) kushindwa kuandaa uchaguzi huru, wa kuaminika na wa wazi.

Kwa sasa, mamlaka zinazohusika na uchaguzi zina kazi ya kuhakikisha zinalinda vifaa vya kupigia kura ambavyo tayari vilishawasilishwa kwenye vituo vya kupigia kura, huku hali ikiwa ya wasiwasi kutokana na matukio ya hivi karibuni ambapo baadhi ya majengo ya tume ya uchaguzi yalichomwa moto.


Comments

comments