Katika kuhakikisha kuwa wakulima wa zao la korosho wanalipwa fedha zao mapema bila usumbufu,serikali imeanza kuwalipa wakulima wa zao hilo wilayni Nanyumbu ambapo zaidi ya shilingi milioni 550 zimeshalipwa


Katika kuhakikisha kuwa wakulima wa zao la korosho wanalipwa fedha zao mapema bila usumbufu,serikali imeanza kuwalipa wakulima wa zao hilo wilayni Nanyumbu ambapo zaidi ya shilingi milioni 550 zimeshalipwa kwa wakulima huku zoezi la malipo likiendelea.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa wilaya ya Tunduru Juma Homera amesema kuwa serikali inaendelea kufanya malipo kwa wakulima wa zao la korosho kwa kuwaingizia fedha kwenye akaunti zao za benki mbalimbali ambapo mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 550 zimeshalipwa huku malipo mengine yakiendelea kufanyika.

Wakulima waliolipwa fedha zao wamemshukuru Rais Dr. Magufuli kwa kuwalipa fedha zao mapema.

Wakati huo huo jeshi la polisi wilayani humo linawashikiria watu kumi na nne wakazi wa wilaya hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya korosho kinyume cha sheria yaani Kangomba ambapo kati yao ni diwani wa kata ya Nalasi Magharibi Khalifa Kabango.

Comments

comments