Wananchi wa Nigeria wanaendelea kusubiri kupiga kura baada ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika siku ya Jumamosi Februari 16 kuahirishwa hadi Jumamosi Februari 23, 2019.

Wananchi wa Nigeria wanaendelea kusubiri kupiga kura baada ya uchaguzi uliokuwa umepangwa kufanyika siku ya Jumamosi Februari 16 kuahirishwa hadi Jumamosi Februari 23, 2019 hatua ambayo imewashangaza wengi huku baadhi wakitilia shaka iwapo uchaguzi huo utakuwa huru,wa kuaminika na wa wazi.

Tume ya uchaguzi nchini Nigeria ilitangaza kuahirisha uchaguzi mkuu kwa juma moja, hatua iliyochukuliwa zikiwa zimesalia saa chache tu kabla ya wananchi wa taifa hilo kuanza kupiga kura.

Tume ya uchaguzi inasema imefikia uamuzi wake baada ya kutafakari kwa kina kuhusu masuala ya usafirishaji wa vifaa na kufika kwa wakati kwenye vituo, changamoto ambayo tume hiyo inasema isingewezekana kuwa na uchaguzi huru, haki na wakuaminika.

Hata hivyo waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi huo wametoa wito kwa raia wa taifa hilo kuwa watulivu wakati maandalizi ya uchaguzi yakiwa yanaendelea.

Comments

comments