Washtakiwa watatu wa makosa ya mauaji ya watoto Njombe wamefikishwa mahakamani na kesi yao kutajwa kwa mara tatu na kisha kuahirishwa hadi Machi 25 Mwaka huu kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

Washtakiwa watatu wa makosa ya mauaji ya watoto GODLIVER, GILIAD na GASPER NZIKU waliokuwa wakazi wa Kijiji cha Ikando, Kata ya Kichiwa wilaya na mkoa wa Njombe wanaokabiliwa na kesi namba moja ya mwaka 2019 leo wamefikishwa mahakamani na kesi yao kutajwa kwa mara tatu na kisha kuahirishwa hadi Machi 25 Mwaka huu kwa kuwa upelelezi haujakamilika.

Aidha mshitakiwa JOEL NZIKU amesomewa shitaka jipya la kupoka mtoto GAUDENCIA KIHOMBO mkazi wa Kijiji cha Ikando, Kata ya Kichiwa mkoani Njombe ambaye hadi sasa hajulikani alipo.

Washiktakiwa hao watatu, JOEL NZIKU, NASSON KADUMA na ALPHONCE DANDA wamefikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka yao na Mwendesha mashitaka wa Serikali, HAPPINES MAKUNGU mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Njombe, MAGDALENA NTANDU ambaye ameahirisha kesi hiyo.

Awali kabla ya washitakiwa hao watatu hawajafikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mkoa wa Njombe, mshitakiwa JOEL NZIKU alisomewa shitaka jipya la kupoka mtoto GAUDENCIA KIHOMBO mwenye umri wa miaka saba, mkazi wa Kijiji cha Ikando, Kata ya Kichiwa mkoani Njombe ambaye hadi sasa hajulikani na wakili wa serikali Elizabeth Mallya mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Njombe, JAMES MHANUSI .

Kwa mujibu wa Mwendesha mashitaka wa serikali, Elizabeth Mallya amesema mshitakiwa JOEL NZIKU anashitakiwa kwa kifungu cha sheria namba 246 na 249 cha kanuni ya adhabu sura namba 16 marejeo ya mwaka 2002 na kueleza shitaka hilo linaruhusiwa kupata dhamana, lakini Hakimu JAMES MHANUSI amesema mshatakiwa haruhusiwi kupata dhamana kwa sasa kwa sababu bado ana mashitaka mengine yayomkabili ya mauaji na hivyo kuamuru arudishwe mahabusu hadi Machi 25, mwaka huu.

Comments

comments