Watoto wawili wa shule ya Msingi Bwawani na Kijichi wilayani Temeke wamefariki dunia huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali baada ya kuangukiwa na Ukuta wakati wakiwa mapumziko

Watoto wawili wa shule ya Msingi Bwawani na Kijichi wilayani Temeke wamefariki dunia huku wengine watatu wakijeruhiwa vibaya na kukimbizwa hospitali baada ya kuangukiwa na Ukuta wakati wakiwa katika mapumziko baada ya kutoka darasani.

Tukio hilo lilileta taharuki katika shule hizo zilizopo jirani na kusababisha wazazi kufurika na kujua hatma za watoto wao.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix lyaniva baada ya kupata taarifa ya Tukio hilo alifika katika shule hizo na kuangalia eneo la tukio,lakini pia alitembelea zahanati ya Mara health care ya kijichi ambapo mmoja wa majeruhi alifikishwa hapo lakini akafariki dunia.

Aidha Bw,Lyaniva alifika katika hospitali ya Mbagala zakhem na kuongea na Mukrim msafiri mwanafunzi wa darasa la pili wa shule ya msingi Bwawani ambaye alinusurika huku akiwa ameumia sehemu ya kichwa na Mkono.

Mkuu wa wilaya ya Temeke Felix lyaniva akizungumza na Chanelten amesema kutokana kadhia hiyo utafanyika Uchunguzi kubaini chanzo cha Kuanguka kwa ukuta huo lakini pia ikibainika kuwa umejengwa chini ya kiwango hatua za kisheria zitachukuliwa kwa waliohusika na ujenzi.

Comments

comments