Kufuatia shambulio lililoua watu zaidi ya 60 katika kambi ya wakimbizi Afrika ya kati.

Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na shirika la habari la AFP imesema serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa baada ya shambulio katika kambi ya wakimbizi ya Alindao Novemba 15, ambapo watu zaidi ya 60 waliuawa.

Timu kadhaa zilikwenda hapo jana katika eneo la tukio ili kujaribu kujua hali halisi na mambo yanayohitajika.Ikiwa idadi ya watu waliouawa bado haijajulikana, mazingira ya tukio hilo pia hayajulikani na hali hiyo imeibua maswali mengi, ikiwa ni pamoja na maswali kuhusu hatua ya Minsuca.

Wengi wanajiuliza jinsi gani tukio hilo liliweza kutokea mbele ya macho ya kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA).

Msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Vladimir Monteiro, amesema mapigano hayo hayakuwa yametarajiwa na idadi ya kikosi cha Umoja wa Matiafa kilikuwa hakitoshi kwa kuzima shambulio hilo.

Viongozi wawili wa kidini ni miongoni mwa waathirika wa kambi hiyo ya Alindao ambapo Baadhi ya watu waliouawa, wengi walichomwa moto na wengine kukatwa katwa.

Comments

comments