Watumishi wawili wa idara ya afya wa Zahanati ya Mutundu Wilaya ya Chato Mkoani Geita wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani humo kwa tuhuma za kuuza na kutorosha dawa za serikali kwa mfanyabiashara mmoja Mkazi wa Buseresere.

Watuhumiwa hao ni Mganga Mfawidhi waa zahanati hiyo Thobias Kagomana, muuguzi Boniface Paschal ambaye pia ni mtunza stoo pamoja na Mfanyabiashara Balamius Kamugisha.

Taarifa za Jeshi la polisi zinasema kuwa Mtuhumiwa Balamius Kamugisha amekamatwa katika Kata ya Buseresere kwa kosa la kukutwa na dawa za Binadamu nyumbani kwake kinyume na sheria, huku ikidaiwa kuwa amekuwa akila njama mara kwa mara na watumishi hao kuhujumu afya za wananchi kama kamanda wa polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo anavyobainiasha.

Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Chato, Dkt. Elibariki Moleli amezitaja dawa zilizokamatwa na jeshi la Polisi, huku Mkuu wa Wilaya hiyo Mtemi Msafiri amesema halmashauri ya Chato inapata dawa zaidi ya asilimia 95.

Comments

comments