Watu Arobaini na tisa wameuawa na wengine zaidi ya ishirini wamejeruhiwa vibaya katika mashambulizi yaliyotokea katika misikiti miwili Christchurch nchini New Zealand.

Waziri mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern ameelezea tukio hilo kuwa ni shambulizi la kigaidi na ni tukio baya kuikumba nchi hiyo.

Maafisa wa polisi nchini humo wamesema wanaume watatu na mwanamke mmoja wanashikiliwa kuhusika na shambulizi hilo na kuonya kuna uwezekano wa kuwepo kwa watuhumiwa wengine zaidi.

Waziri mkuu wa Australia Scott Morrison amesema kati ya walioshikiliwa ni raia wa nchi yake, ameumuelezea mtu huyo kuwa gaidi mwenye msimamo mkali wa mrengo wa kulia.

Comments

comments