Wakati dunia ikiadhimisha siku ya UKIMWI leo, ikiwa ni maadimisho ya 30, shirika la afya duniani WHO, limesema watu milioni 37 duniani wanaishi na maambukizi ya virusi vya UKIMWI huku vijana wakiendelea kuwa hatarini zaidi kuambukizwa hasa barani Afrika.

Uchunguzi wa WHO umebaini kuwa asilimia 71 ya maambukizi mapya yanatokea barani Afrika, hasa eneo la Afrika Mashariki na Kusini mwa bara hili.

Watu wengine milioni 22 waliombukizwa wanatumia dawa za ARV’s ambazo zinasaidia kudumaza virusi hivyo.

Siku ya kimwi duniani hutumiwa na wanaharakati na wakuu wa nchi, kutoa elimu kuhusu namna ya kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kupiga vita unyanyapaa na kuhimiza watu kufanya vipimo ili kufahamu hali zao.

Woga, unyanyapaa na kupuuza ni mambo unayoendelea kuitesa dunia katika mapambano ya ugonjwa huo ambao umesbabisha vifo vya mamilioni ya watu tangu miaka ya 1980.

Comments

comments