Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa ngazi ya klabu, Timu ya Simba ya DSM leo watakuwa Uwanja wa Taifa wakitafuta pointi muhimu mbele ya timu ya Al Ahly ya Misri.

Mchezo huo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni wa mzunguko wa nne na mpaka sasa hakuna timu ambayo ina uhakika wa kwenda robo fainali kwenye kundi lao la D.

Simba ipo Kundi D ikiwa na timu za Al Ahly iliyo kileleni na pointi saba, AS Vita ya CONGO DRC yenyewe ni ya pili ikiwa na pointi nne, wakati Simba ya tatu ikiwa na alama tatu na ya mwisho ni JS Saoura ya Algeria yenye alama mbili.

Simba imefungwa kwenye michezo miwili iliyopita kwa mabao 5-0 kila mechi, ilianza kufungwa na AS Vita kule Congo DRC na baadaye ikapokea kipigo kama hicho Misri mbele ya Al Ahly

Simba itakuwa inaingia uwanjani leo kwa lengo la kusahihisha makosa yaliyojitokeza kwenye mechi mbili zilizopita kwa kuhakikisha wanapata ushindi utakaofufua matumaini zaidi ya kwenda robo fainali kisha hatua itakayofuata.

Comments

comments