Uingereza inatarajiwa kuikalia kooni Saudi Arabia,kuhusiana na mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi

Uingereza inatarajiwa kuikalia kooni Saudi Arabia,kuhusiana na mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi na Operesheni yake ya kijeshi nchini Yemen.

Waziri Mkuu wa Uingereza,Theresa May,amewaambia waandishi wa habari akiwa njiani kuelekea Buenos Aires,Argentina,kwenye mkutano wa nchi 20 zenye viwanda na zinazoinukia,kuwa amenuia kuzungumza na mrithi wa mfalme wa Saudia Mohammed bin Salman,kuhusiana na masuala hayo mawili.

Bi May,amesema hatakuwa na kigugumizi mbele ya Mohammed bin Salman,maarufu kama MBS,kuwa msimamo wa Uingereza ni kutaka uwazi katika uchunguzi wa suala la Kashogi na kuwajibishwa wote waliohusika katika mauaji hayo.

Nchi za Magharibi zinaitolea wito Saudi Arabia,kuhitimisha kampeni yake ya kijeshi nchini Yemen,kufutia kuendelea kuzorota kwa hali ya kibinadamu nchini humo na kwamba suluhu ya muda mrefu ya suala la Yemeni,litapatikana kisiasa.

Comments

comments