Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema wizara hiyo inaendesha Kampeni ya kutoa elimu nchi nzima kwa vijana ili vijana hao waweze kukuza vipaji vyao pamoja na kuwa na weledi katika utengenezaji wa picha za filamu.

Dkt. Mwakyembe ameyasema hayo katika Mji mdogo wa Nduguti,wilayani Mkalama baada ya kupokea taarifa ya wilaya hiyo iliyoonyesha jitihada za kulikarabati jengo la Boma la Mjerumani na kubaini pia kuwa wilaya ya Mkalala bado ipo nyuma katika masuala ya utengenezaji wa picha za filamu na ndipo akatoa ahadi kwa wana – Mkalama.

Aidha Dkt. Mwakyembe amesema kwamba Tanzania kwa mwaka inazalisha zaidi ya picha za sinema 1,500 ambazo idadi kubwa zimekuwa na weledi na picha chache tu ndizo zimekuwa zikichomoza kuwa bora na kuiwezesha Tanzania kushinda katika tuzo nyingi.

Awali akitoa taarifa ya wilaya ya Mkalama kwa waziri huyo, Mkuu wa wilaya ya Mkalama, ENG. JACKSONI MASAKA amesema jengo la Boma la Mjerumani lililopo Kijiji cha Mkalama limejengwa kuanzia mwaka 1904 hadi 1910 kwa kutumia mawe, udongo na saruji na lilitumika kwa utawala wa kikoloni pamoja na shughuli za uzalishajimali kwa wakati huo.

Comments

comments