Waziri Mkuu azindua wiki ya Uwekezaji.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amezindua wiki ya uwekezaji mkoa wa Kagera na mwongozo wa uwekezaji katika mkoa huo kwa kuwaomba wawekezaji kutoka nje ya nchi kuchagamkia fursa zilizoko nchini baada ya vikwazo vilivyokuwepo hapo awali kuondolewa.

Akifungua mwongozo huo Waziri Mkuu amesema kuwa hivi sasa mtu anayetaka kuwekeza nchini anaweza kuanza mchakato akiwa popote kupitia mfumo wa tehama unaowezesha vitu vingi vya uwekezaji kufanyika kwa njia ya mtandao.

Mapema Mkuu wa mkoa Kagera Breg Gener Marco Gaguti amesema maeneo makubwa ya uwekezaji yapo katika sekta za kilimo,utalii,ufugaji,uvuvi,viwanda,misitu,madidini nabhuduma za kijamii.

Wiki ya uwekezaji Kagera iliyoanza august 12 mwaka huu itahuitishwa august 17 mwaka huu ambapo shughuli mbalimbali ikiwemo kutambua maeneo ya uwekezaji ,namna ya kuwekeza yanajadaliwa na wadau kuoanga namna ya kuwekeza katika maeneo hayo.

Comments

comments