Waziri Kakunda, amewahimiza Watanzania kupanda mazao yanayoondoa umasikini ikiwemo Miparachichi, kwani ukiweza kulima zao hilo unaweza kuvuna katika maisha yako yote.

Waziri wa Viwanda na Biashara Joseph Kakunda, amewahimiza Watanzania kupanda mazao yanayoondoa umasikini ikiwemo Miparachichi, kwani ukiweza kulima zao hilo unaweza kuvuna katika maisha yako yote.

Waziri Kakunda akiendelea na ziara yake Wilayani Siha Mkoani Kilimanjaro, alipata fursa ya kutembelea Kiwanda cha Africado, kinachozalisha miparachichi , ambapo amewahamasisha watanzania kujijengea utaratibu wa uthubutu kwa kununua miche ya miparachichi kutoka katika kiwanda hicho, ili kuizalisha na kupata faida kubwa katika maisha yao.

Aidha Waziri Kakunda ameagiza miradi yote ya huduma za jamii iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara wapewe halmashauri agizo ambalo amesema halina mjadala.

Mkuu wa Wilaya ya Siha kwa upande wake ameupongeza uongozi wa Kiwanda cha Africado kwa kuwa mlipaji mkubwa wa kodi za serikali ikilinganishwa na wawekezaji wengine na ametumia fursa hiyo kuiomba serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji hapa nchini.

Comments

comments