Wizara ya Madini kwa kushirikiana na Taasisi ya uongozi nchini, imewakutanisha wadau wa sekta ya madini kujadili kanuni za Sheria ya madini ya mwaka 2017, ili rasilimali hiyo iweze kuwanufaisha Watanzania.


Katika kikao hicho kinachoketi Jijini Mwanza, shabaha kubwa inalenga kuimarisha soko la Madini, ili rasilimali hiyo iweze kuchangia kikamilifu katika pato la Taifa, baada ya kubainika kuwa bado kuna wimbi kubwa la utoroshaji wa madini hapa nchini.

Kutokana na mjadala huo inategemewa kuwa, hii itakuwa ni neema kwa wachimbaji wadogo pia kupata soko la uhakika, baada ya marekebisho ya sheria hiyo kuwalegezea tozo ya kodi, iliyokuwa ikitajwa kama chanzo cha utoroshaji wa madini hayo.

Simon Msanjila ni Katibu mkuu wa Wizara ya Madini, anayataja maeneo ambayo yanajadiliwa ndani ya kikao hiki, ambacho ni cha mhimu kwa wadau hao kutoa maoni yao, ili waweze kuonja ladha ya mafanikio katika biashara ya sekta ya Madini.

Kama ilivyo kawaida ya wachimbaji wadogo panapo jambo huketi kando kunena yao, ambapo nje ya mkutano huo, wamekutana na waandishi wa habari na kisha kukata kiu yao, kwa kubainisha faida za maboresho ya kanuni ya sheria ya Madini.

Comments

comments