Xi na Trump wakubaliana kuacha kuongeza ushuru wa forodha

Marais wa China na Marekani wamekubaliana kuacha hatua za kutozana ushuru nyongeza wa forodha.

Hayo yametangazwa na waziri wa mambo ya nje wa China Wang Yi baada ya mazungumzo kufanyika kati ya rais Xi Jinping na rais Donald Trump Jumamosi jioni huko Buenos Aires, Argentina.
Marais hao walijadili masuala ya uchumi na biashara, na kufikia makubaliano muhimu, huku walitoa mapendekezo kadhaa na kadhaa kuhusu namna ya kuondoa tofauti na kutatua masuali yaliyopo. Kwa upande wa China, katika juhudi za kuleta uwiano wa kibiashara, inapenda kuagiza bidhaa za Marekani zinazolingana na mahitaji ya soko na wateja wa China. Na marais hao walikubaliana kila nchi kufungua soko lake kwa nchi nyingine, na matakwa yenye haki ya Marekani yatazingatiwa katika mchakato wa China kuendeleza sera ya mageuzi na mlango wazi. Maofisa wa nchi mbili watafanya mazungumzo haraka kwa msingi wa yaliyofikiwa na marais wao, ili kufikia makubaliano halisi mapema kwa lengo la ushuru wa nyongeza wa forodha uondolewe kabisa.
Rais Xi Jinping na rais Donald Trump walikuwa na chakula cha jioni kwa pamoja na kufanya mazungumzo ya masaa mawili na nusu Jumamosi jioni, huko Buenos Aires. Makutano yaliyopita kati ya marais hao yalifanyika mwezi Novemba mwaka jana huko Beijing.
Habari zinasema pande zote mbili zinaona makubaliano ya kikanuni yaliyofikiwa katika mazungumzo hayo yana maana kubwa, kwamba yanazuia mikwaruzano ya kibiashara isizidi kuwa mibaya zaidi, na kuleta matumaini mapya ya ushirikiano unaonufaishana, hali ambayo si kama tu inasaidia maendeleo ya China na Marekani na kulingana na manufaa ya watu wao, bali pia inachangia ongezeko la uchumi wa dunia na manufaa ya nchi mbalimbali.
Kwenye mazungumzo hayo, marais hao pia walijadili masuala mengine yakiwemo kuimarisha ushirikiano katika kupambana na dawa za kulevya, na hali ya peninsula ya Korea. China imerudia msimamo wake wa kikanuni kuhusu suala la Taiwan, na Marekani imesisitiza kushikilia sera ya kuwepo kwa China moja.

Comments

comments