Barabara Jimbo la Ukonga Ilala Zakarabatiwa.

Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini dsm imeanza kuziboresha barabara zilizoharibika vibaya kutokana na mvua na kusababisha kupitika kwa shida katika mitaa mbali mbali ya Jimbo la ukonga.

Akizungumza na Waandishi wa habari Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala Omar Kumbilamoto amesema Ukarabati huo ambao ulisimama kwa zaidi ya wiki mbili kutokana na kuharibika kwa baadhi ya vifaa ikiwemo betri sasa Umepatiwa ufumbuzi na kazi ya kurekebisha barabara hizo unaendelea.

Aidha Kumbilamoto amemtaka Mkandarasi wa Manispaa hiyo pamoja na timu yake kuhakikisha barabara hizo zinafanyiwa marekebisho ya haraka huku pia akiwasiliana na Tarura ili kuzifanyia matengenezo makubwa ili zipunguze adha na Shida kwa wananchi wengi wananaotumia barabara hizo.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Taarifa ya Habari ya Saa Moja Kamili Usiku channel Ten

Read Next

Mkutano wa Rais Mhe. Dkt. Magufuli na Watendaji wa Kata Nchini.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!