Waziri Mkuu wa Sudan Kutangaza Baraza la Mawaziri.

Waziri Mkuu mpya wa Sudan Abdalla Hamdok amefanya mazungumzo ya kuunda baraza la kwanza la mawaziri tangu Omar al-Bashir alipoondolewa madarakani.

Hamdok alitarajiwa kutangaza baraza la mawaziri baada ya Baraza la Mpito linalowajumuisha wajumbe wa kiraia na kijeshi kuapishwa wiki iliyopita.

Baraza hilo litakuwa na mawaziri 20 wengi wao watateuliwa na bwana Hamdok. Lakini mawaziri wa mambo ya ndani na ulinzi watachaguliwa na wajumbe wa kijeshi wa baraza hilo la mpito.

Waziri Mkuu huyo mpya ameahidi kukomesha vita na kuleta amani ya kudumu nchini Sudan.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Mkutano wa Rais Mhe. Dkt. Magufuli na Watendaji wa Kata Nchini.

Read Next

Mashambulizi ya Angani Eneo la Idlib Syria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!