Watu zaidi ya nane wamefariki dunia hapo jana huku wengine zaidi ya 26 wakiwa hawajulikani walipo katika mkasa wa moto mkubwa uliozuka katika meli ya watalii kwenye pwani ya California.
Hata hivyo mamlaka katika mji wa Barbara, katika Jimbo la California, ambako tukio hilo limetokea, wanahofu kuwa idadi hiyo inaweza kuongezeka na kuwa kubwa zaidi kuliko ilivyotarajiwa. Meli hiyo ilikuwa ikisafiri karibu na kisiwa cha Santa Cruz, ambapo watalii walikuwa katika zoezi la kupiga mbizi.
Vyanzo kutoka idara ya huduma za dharura, vinabaini kwamba watu 39 walikuwa wakisafiri katikameli hiyo ambapo vyanzo hivyo vimeongeza kuwa miili minne ya watu waliofariki imeopolewa kutoka majini ikiwa ni wanawake wawili na wanaume wawili ambao bado hawajatambuliwa rasmi huku miili mingine miwili ikionekana chini ya bahari karibu na Meli
Akizunguza katika tukio la uokoaji Kiongozi wa Huduma ya dharula Bill Brown amesema mpaka sasa wana timu za wapiga mbizi, ambao wanajaribu kuopoa miili hiyo, lakini amesema bado kazi ni nzito na hawana uhakika uhakika kama wataweza kuopoa miili hiyo ambayo imekwama baharini.