Mashambulizi ya Angani Eneo la Idlib Syria.

Majeshi ya Urusi na Marekani yameanzisha mashambulizi ya angani katika eneo la Idlib nchini Syria bila kuionya Uturuki na kuhatarisha mkataba wa kusitisha mapigano. Haya yameripotiwa leo Jumapili na shirika la habari la Urusi.

Shirika la habari la TASS limemnukuu waziri wa ulinzi wa Urusi akisema kuwa mashambulizi hayo yamekiuka makubaliano ya awali na kusababisha majeruhi wengi.

Kituo hicho kimeripoti kuwa ndege za kivita za Urusi na Syria zilikuwa zimeahirisha kikamilifu mashambulizi dhidi ya wanamgambo katika mkoa wa Idlib Kaskazini Magharibi mwa Syria baada ya kutangaza kusitisha mapigano yalioanza siku ya Jumamosi asubuhi.

Chini ya mkataba na Urusi na Iran, jeshi la Uturuki lina vituo kadhaa katika eneo la Idlib .

Uturuki pia inaunga mkono vikosi vya waasi vinavoyshikilia ngome kadhaa Kaskazini mwa Idlib karibu na mpaka wake.

Comments

comments

Clement Silla

Read Previous

Waziri Mkuu wa Sudan Kutangaza Baraza la Mawaziri.

Read Next

Watu wengi wafariki Dunia katika Meli Mjini California.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Follow On Instagram
error: Content is protected !!